Uzuri wa Gereza Hazina iliyosahaulika (Kiswahili Sehemu ya 1)
Uzuri wa Gereza Hazina iliyosahaulika (Kiswahili Sehemu ya 1)
Hapa ulimwenguni kuna vitabu vichache sana ambavyo mkono wa mwandishi huingia, huchokonoa na
kudondosha tone la NURU katika kilindi cha moyo wako wewe msomaji na kukumurikia mwanga
wenye kuleta mabadiliko chanya katika maisha yako binafsi ya kila siku, Kitiabu hiki ni utekelezaji wa
makusudi ya Mungu katika kuanzisha, kustawisha na kudhihirisha UAMSHO wenye kuleta mapinduzi
makubwa ya kiroho, kijamii, kiutamaduni, kiuchumi na kiujasiriamali kwa kutumia rasimali watu nchini
Tanzania, Afrika Mashariki (EAC) na Nchi za ukanda wa maendeleo kusini mwa bara la Afrika (SADC),
Hivyo basi kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu vichache vyenye sifa hiyo adhimu.