Shughuli za Anna za Kila Siku
Shughuli za kila siku za Anna ni kitabu kinachoeleza Anna anavyofanya shughuli zake za kila siku kwa utaratibu mzuri. Shughuli hizi zimepangwa kufuatana na alfabeti. Kila herufi ya alfabeti inayo shughuli yake maalumu kwa Anna na wenzake.
Madhumuni ya kuandika kitabu hiki ni kufundisha maadili mema mtoto tukitilia maanani methali ya Kiswahili isemayo, “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.” Nia ni maadili haya yawe mfano wa kuigwa na watoto wetu wakiwa bado wadogo. Kila mwisho wa ukurasa kuna swali la kujibu.
Mwishoni mwa kitabu kuna zoezi.
Walengwa wa kitabu hiki ni wanafunzi wa Shule za Msingi.
ISBN 978-9987-671-49-6
| Weight | 500g |